Bi Rashida Tlaib, mwakilishi wa jimbo la Michigan wa chama cha Democrat katika Bunge la Wawakilishi la Marekani leo ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba: Jinai mpya za utawala wa Kizayuni huko Khan Yunis na kunyamaza kimya viongozi wa dunia mbele ya jinai hizo ni jambo la kuhuzunisha, na ameiomba mahakama ya ICC iamuru kutiwa nguvuni wahusika wa mauaji hayo ya kimbari.
Mwakilishi huyo wa chama cha Democratic nchini Marekani ameongeza kuwa: Israel imewashambulia kwa makusudi raia wa Palestina mara chungu nzima na viongozi wa dunia wanatazama tu jinai hizo za Israel na hawachukui hatua yoyote. Amesema, hata baadhi yao wanaendelea kufadhili jinai hizo za kinyama za Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Utawala wa Kizayuni wa Israel jana Jumanne ulishambulia shule ya al Awda katika kitongoji cha Absan mashariki mwa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza na kutenda jinai nyingine dhidi ya Wapalestina. Habari zinasema kuwa Wapalestina wasiopuungua 29 wameuawa shahidi katika hujuma hiyo ya kikatili ya Israel.
342/